사랑하는교회

전체메뉴보기 검색
통합검색 검색

교회소식

최신소식

목록보기

지저스디바인 크리스마스 앨범(찬송가 4곡) 스와힐리어 Ver.

담대 |

2025-12-31 13:08:39 |

조회: 11

할렐루야!

기존 지저스디바인 크리스마스 앨범에 수록된 MR과

또 AI 보컬을 활용해서 아프리카에서 많이 쓰는 언어인

스와힐리어로 찬송가 4곡을 제작해 보았습니다^^

 

아프리카를 위해 중보하는 마음으로

함께 들어주시면 감사하겠습니다!^^

 

https://youtu.be/gLQne-F50uA?list=RDgLQne-F50uA

<소개글>

 

Kutoka Korea Kusini, tunawaletea salamu za upendo na furaha.

Heri ya Krismasi!  - JESUSDIVINE.

 

 대한민국에서 사랑과 기쁨의 인사를 전합니다.

메리 크리스마스!  - JESUSDIVINE

 

 From South Korea, we bring you greetings of love and joy.

Merry Christmas!  - JESUSDIVINE.

 

01 Mbali Kule Nasikia (Angels We Have Heard on High)

02 Furaha Kwa Ulimwengu (Joy to the World)

03 Mungu ni wa utukufu (Hark! The Herald Angels Sing)

04 Njooni, Enyi Wa Imani (O Come, All Ye Faithful)

 

 

01 Mbali Kule Nasikia (Angels We Have Heard on High)

 

Mbali kule nasikia malaika wa mbinguni,Wakiimba wengi pia wimbo huo juu angani:Gloria in excelsis Deo,Gloria in excelsis Deo.

 

Wachunga tuambieni sababu ya nyimbo hizo?Mwenye kuimbiwa ni nani, juu ya nani sifa hizo?

 

Je hamjui jambo kuu la kuzaliwa Mwokozi?Habari ya wimbo huo ndiyo kumshukuru Mwenyezi.

 

Kweli, nasi twende hima, tufike kule aliko,Tuone mtoto na mama, tuwasalimie huko

 

 

02 Furaha Kwa Ulimwengu (Joy to the World)

 

Furaha kwa ulimwengu!

Bwana amekuja;

Nyote mkaribisheni,

Mioyo yenu na mpeni;

Wote wanshangilie,

Wote wanshangilie,

Na wote, na wote wamshangilie.

 

Furaha kwake dunia!

Mwokozi ni Mfalme;

Bonde mlima na mwamba,

Maji mitoni na shamba,

Rudisheni sauti,

Rudisheni sauti,

Rudisheni, na rudisheni sauti.

 

Dhambi zisiongezeke,

Wala wahalifu;

Yuaja kutubariki,

Atuletea ushindi;

Kuharibu dhambi,

Kuharibu dhambi,

Na kuharibu, na kuharibu dhambi.

 

Atawala na neema,

Kwao mataifa;

Utukufu na waone,

Haki yake itendeke;

Kwa upendo wake,

Kwa upendo wake,

Kwa upendo, na kwa upendo wake.

 

 

03 Mungu ni wa utukufu (Hark! The Herald Angels Sing)

 

Waimba, sikizeni,

Malaika mbinguni;

Wimbo wa tamu sana

Wa pendo zake Bwana;

"Duniani salama,

Kwa wakosa rehema."

Sisi sote na twimbe

Nao wale wajumbe;

Waimba, sikizeni,

Malaika mbinguni.

 

Ndiye Bwana wa mbingu,

Tangu milele Mungu,

Amezaliwa mwili,

Mwana wa mwanamwali;

Ametoka enzini

Kuja ulimwenguni

Mwokozi atufie,

Ili tusipotee,

Waimba, sikizeni,

Malaika mbinguni.

 

Seyidi wa amani

Ametoka Mbinguni,

Jua la haki, ndite

Atumulikiaye;

Amejivua enzi,

Alivyo na mapenzi,

Ataka kutuponya,

Kutuzalisha upya,

Waimba, sikizeni,

Malaika mbinguni.

 

Njoo upesi, Bwana,

Twakutamani sana;

Kaa nasi, Mwokosi,

Vita hatuviwezi;

Vunja kichwa cha nyoka,

Sura zako andika,

Tufanane na Wewe,

Kwetu sifa upewe,

Waimba, sikizeni,

Malaika mbinguni.

 

 

04 Njooni, Enyi Wa Imani (O Come, All Ye Faithful)

 

Njoni na furaha, Enyi wa Imani,

Njoni Bethlehemu upesi!

Amezaliwa mjumbe wa Mbinguni

Njoni tumuabudu, Njoni tumuabudu,

Njoni tumuabudu Mwokozi.

 

Mungu wa waungu, Mwanga wa mianga,

Amekuwa radhi kuzaliwa;

Mungu wa kweli, wala si kiumbe

Njoni tumuabudu, Njoni tumuabudu,

Njoni tumuabudu Mwokozi.

 

Jeshi la mbinguni, Imbeni kwa nguvu!

Mbingu zote na zijae sifa!

Sifuni Mungu aliye mbinguni;

Njoni tumuabudu, Njoni tumuabudu,

Njoni tumuabudu Mwokozi.

 

Ewe Bwana Mwema, Twakubarikia,

Yesu, utukufu uwe wako;

Neno la Baba limekuwa mwili;

Njoni tumuabudu, Njoni tumuabudu,

Njoni tumuabudu Mwokozi.

 

 

** Uimbaji umetengenezwa kwa msaada wa teknolojia ya AI.

** The vocals were produced using AI technology.

** 보컬은 AI를 이용해 제작되었습니다.

다음글 강력 추천!!!!!! "성경을 연구하다가 곁길로 빠져서 이단이나 사이비가 되지 않으려면 어떻게 해야 하는가?"(질의응답, 변승우 학장) 사랑하는교회 2025-12-31 13:09:31
이전글 강력 추천!!!!!! "요셉이 보여준 최고의 믿음!"(25. 12. 14. 학생회, 박세훈 목사) 겸손 2025-12-31 13:07:46

공유하기 닫기

url로 공유시 전체 선택하여 복사하세요.